Thursday, August 12, 2010

15 Agosti: Kupalizwa Mbinguni kwa Mama Maria

15 Agosti: Kupalizwa Mbinguni kwa Mama Maria
Insha: Moyo Wangu Wamtukuza Bwana
Masomo: Ufunuo 11:19; 12:1-6,10; 1 Kor. 15:20-26; Luka 1:39-56

Kwenye siku kuu ya kupalizwa mbinguni kwa Maria, tunaadhimisha matumaini yetu ya kwamba nasi pia siku moja tutamfuata yule Mama wetu mbinguni. Basi pamoja na Mama wetu Maria tunamtukuza Bwana. Kuna sinema moja iliyotungwa kuonyesha jinsi jumuiya moja iliharibiwa kabisa na mtetemeko wa ardhi. Sinema hiyo hapo mwisho badala ya kuonyesha “The End” kama kawaida, ilionyesha “The Beginning” (Mwanzo), kwa sababu maisha ya jumuiya ile yalianza upya. Tungesema kwamba mwisho wa maisha ya uaminifu wa Mama Maria hapa duniani ndio ulikuwa mwanzo wa maisha mapya ya kutuombea mbinguni. Basi Kupalizwa mbinguni kwa Mama Maria, kwatuonyesha kwamba ukombozi mkamilififu katika Kristo umeakikishwa kwa kila binadamu. Pale Mama Maria amekwenda, sisi zote twategemea kufika. Kwenye Injili, tunaona Maria akimtembelea na kumsalimia binamu yake Elizabeti. Kwa kweli ni safari ya imani inaotuonyesha jinsi Maria alikuwa ameelewa kabisa kwamba Mungu amembariki. Baraka hizi zaambata na utukufu wa Mwanao Yesu Kristo. Akiongozwa na Roho Mtakatifu, Elizabeti anaakikisha baraka hizi. Tunaadhimisha siku kuu ya Kipalizwa Mbinguni ili kuonyesha uhusiano wa Mama Maria na Mwanae kwenye utukufu wake. "Umebarikiwa kuliko wanawake wote, yeye utakayemzaa amebarikiwa" (Lk. 1:42). Mama Maria amebarikiwa kwa sababu Mwanae amebarikiwa na Baba. Pia yumo kwenye mahali asili kwenye Kanisa kwa sababu ya imani yake katika Mungu. Kwa imani hiyo, Maria alikaribisha ujumbe wa Malaika Kabrieli alipokuja kumpasha habari ya kwamba angekuwa Mama wa Mungu. “Amebarikiwa yeye aliye amini kwamba lile Bwana alilomwambia litatimizwa” (Lk. 1:45). Ndiyo sababu Maria anamtukuza Bwana moyoni mwake kwa ajili ya Baraka aliyopewa.

Safari hiyo ya imani, iliyokomea kwa Kupalizwa kwake Mbinguni, yaonyeshwa kwenye uelewaji wake wa kindani wa jinsi Mungu amemteua. Ndiyo sababu Maria, kwenye Injili ya leo anaimba ule wimbo wa kumtukuza Bwana wakati wa kumtembelea Elizabeti. Kwnye ule mkutano wa maana, Maria anatafakari mbele ya Mungu, anyeangalia kwa fadhili unyonge wa mtumishi wake. Lakini kile kilicho maana sana ni mahali pa Maria katika Kanisa kwa sababu ya imani yake kuu katika Mungu. Kwa imani hii Maria alipokea ujumbe wa kuwa Mama wa Mungu. "Heri yako wewe uliyesadiki kwamba yatatimia yale Bwana aliyokuambia" (Lk.1:45). Kwa kweli Maria alikuwa safarini ya imani wakati wote, akiidumisha kika mara maishani mwake, kuelekea Msalabani hadi kufufuka kwa Mwanao. Imkani hii ilimwongoza Maria kuimba kwa furaha utenzi wake kwa Bwana, alipomtembelea Elizabeti. Kuna ujumbe gani tungepeleka nyumbani Jumapili hii? 1) Mwisho wa maisha ya uaminifu wa Mama Maria waanzisha upya maisha ya kutuombea mbinguni kwa Mwanae Yesu; 2) Kama tunavyosikia kwenye Somo la Kwanza, Maria ndiye yule Mwanamke aliyevyeka Jua na Mwezi miguuni, akivyeka taji ya nyota kumi na mbili kichwani. Kule kuepuka kuuawa na joka mkubwa, ni ishara ya jinsi Maria yumo karibu nasi kwenye vita vya maisha yetu hapa duniani hadi mwisho; 3) Maisha ya Mama Maria ni akikisho ya kwamba ukombozi umehahidiwa kwa kila binadamu, kwa sababu pake Mama amekwenda, twategemea nasi kufika.

©2010 John S. Mbinda

No comments: