Friday, May 14, 2010

16 Mei: Kupaa kwa Bwana Mwaka C

16 Mei: Kupaa kwa Bwana Mwaka C
Inshaa: Akapaa Mbinguni, Ameketi kuume kwa Baba
Masomo: Matendo 1:1-11; Waefeso 1:17-23; Lk 24: 46-53

Jumapili hii tunaadhimisha siku kuu ya Kupaa mbinguni kwa Bwana. Kwenye Kanuni ya Imani tunasadiki Kristo aliyepaa mbinguni na, "ameketi kuume kwa Baba", maneno ambao hutukumbusha kupaa kwa Bwana kwenye kuume kwa Baba. Ni lazima tuelewe na sikukuu ya Kupaa Mbinguni kwa Bwana katika nuru ya fumbo la Pasaka ya Kristo, ambaye kwa ufufuko wake amepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Lakini kupaa mbinguni kwa Kristo kuna maana gani katika imani yetu na maisha ya Kikrito? Maana yake ni kwamba, Bwana aliyefufuka sasa amewekwa kuume kwa Baba mbinguni, maneno ambao yatuonyesha Baba akimtukuza Kristo Mwanae kwa kumfanya Bwana wa viumbe vyote, na akimpatia "mamlaka yote mbinguni na duniani" (Mathayo 28:18). Tukiangalia masomo ya Jumapili hii tutaona kwamba mitume wa Yesu hawakuelewa kikamilifu umaana wa kupaa mbinguni kwa Yesu. Twaweza kusema kwamba mitume baada ya kuwa na Yesu kwa miaka 3, hawakuelewa na shabaha ya kuja kwake dunia. Walidhani alikuwa kuwakomboa Mayahudi kutokana na ukoloni wa Kirumi. Pia wakati huo wa kupaa mbinguni, mitume wanaonekana wakiangalia mbinguni kwa wakishangaa. Hawajui wafanyeji baadaye. Wakati huo wa kupaa mbinguni kwa Yesu ulikuwa wakati kutafakari.

Kule kuangalia mbinguni kwa mitume ni mfano wa jinsi sisi pia wa leo hatuelewi na shabaha la ujumbe wa Yesu wa kutukomboa na pia umaana wa shabaha la utume wa Kanisa. Yesu aliwashauri mitume wake warudi Yerusalemu na kungojea huko agano la Baba. Yaani wasiende peke yao au kufanya kazi kwa kufuata azimio la ki-mtu. Bali warudie kiasili cha kuisikiliza neno la Mungu na sauti lake kupitia kwa yule Roho Mtakatifu. Katika lugha ya imani, kupaa mbinguni maana yake ni kuingia kikamilifu kwenye utukufu wa Baba. Kwa kufanya hivyo, Kristo hutuwezesha nasi pia tulio viungo vya mwili wake, yaani Kanisa, kumfuata mahali alipo. Pia kuingia kikamilifu kwenye utukufu wa Baba uwezesha Kanisa kupokea Roho Mtakatifu, ambaye huakikisha kuwepo kwa Bwana pamoja nasi daima. Mtk. Paulo alielewa na kupaa kwa Bwana kama kupewa mamlaka yote juu ya viumbe vyote na hasa juu ya pepo wabofu wote, kwa sababu Baba "amevitia vitu vyote chini ya miguu ya Kristo". Kuna ujumbe gani tungepeleka nyumbani? 1) Ujumbe wa siku kuu ya Kupaa Mbinguni kwa Bwana wagusa hasa jinsi tunavyoelewa na shabaha la utume wa Kanisa leo; utume wa upatanisho, usameheo na ugeuzaji wa dunia hii chini ya Ufalme wa Yesu Kristo; 2) Papa Yohane Paulo II alisema kwamba kabla ya kufanya azimio la jimbo yatulazimu kwanza kugojea Yerusalemu. Maana yake tusubiri katika sala, tumsikilize Bwana, ili tujue azimio lake kwanza, na ndipo tutakapotengeneza azimio la jimbo kulingana na yake. 3) Ni kupitia sala tu tutakapofaulu kutekeleza ujumbe wa Yesu, tukishasikiliza jinsi Mungu angependa tufanye.

©2010 John S. Mbinda

No comments: